Jumatano, 11 Desemba 2019

Mambo 6 ya kufanya kama msichana hajibu sms zako


Umekuwa ukimtumia jumbe (sms) msichana, umetumia emojis, memes, umefikiria jina zuri la utani (a.k.a) kwa ajili yake lakini bado hujaambulia jibu katika yote uliyoyafanya.
Unaweza ukawa umekaa unatafakari ni kitu gani ulichokosea kilichosababisha mrembo huyo asikujibu. Unawaza ni namna gani utaweza kukabiliana na hali hii kwani kila simu yako ikiita, unatamani awe ni yeye, kumbe wakati mwingine ni sms za kukumbushwa kwenda kusajili laini kwa alama ya vidole.
Kuna njia mbalimbali za kukabiliana na hali hii, lakini kabla hatujajadili hilo, embu jiulize swali moja, kwanini hajibu sms zangu?
Pengine ametingwa na shughuli zake, au ni mtu ambaye hapendi kutuma sms/hapendi kuchat sana. Lakini hapana, kutuma sms kunachukua sekunde chache sana, kiasi kwamba hakuwezi kumuharibia lolote kwenye ratiba yake.
Sasa je, kama hajibu unafanyaje?
Weka umbali kidogo
Kama msichana hakujibu sms zako, suluhisho sio kumbambikizia lundo la sms, kwa sababu kama hakujibu ujumbe mmoja, usidhani kuwa ukimtumia jumbe 100 basi ndio atajibu, zaidi atakublock, sababu ataona usumbufu.
Kubwa unalotakiwa kufanya hapa ni kupunguza mawasiliano, piga hatua moja nyuma, jioneshe kwa haujali. Fahamu kuwa, matunda yakiwa mengi sokoni, bei hushuka, lakini yakiwa machache bei huwa juu, hivyo lengo hapa ni kupandisha bei yako, hivyo usijioneshe sana, kuwa kila mara upo.
Upungufu utatengeneza uhitaji mkubwa.,
…Usiweke umbali mkubwa sana
Tulichojadili hapo juu haimaanishi kwamba ndio umsahau, hapana, mawasiliano lazima yawepo. Usiache zipite siku 2 au 3 bila kumtumia ujumbe japp mmoja.
Lazima uhakikisha suala la muendelezo (consistency) linakuwepo, maana ni moja ya vitu ambavyo wasichana/wanawake wanapenda sana. Haijalishi kuwa utakuwa unaandika nini kwenye ujumbe wako (ila isiwe tusi) lakini kwa vile kila mara utakuwa unamtumia, hilo linatosha.
Usiulize kwanini hajibu sms zako
Sheria ya msingi, usimuulize kwanini jana au juzi au wakati fulani nilikutumia ujumbe huu na huu lakini hukunijibu. Ukimuuliza itamuonesha kuwa yeye kuto kukujibu kulikuumiza au kulikusononesha. Lengo hapa ni kuonekana mkakamavu, na kwamba yeye kutokukujibu hakukusumbua kabisa.
Mfano ukimtumia ujumbe kumuuliza anafanya nini, lakini hakukujibu, baadae akaleta mada nyingine, usimkumbushe ule ujumbe ambao hakuujibu.
Kamwe usifanye japo kwa utani kumuuliza kuhusu yeye kutokukujibu, kama hakujibu, acha ipite, kikubwa uhai.
Chagua mada mpya ya mazungumzo
Ukimtumia ujumbe leo, asipokujibu, utakapokuja kumtumia tena kesho, usimtumie kuhusu jambo lile lile ulilotuma jana, chagua suala jingine la kuzungumzia, kwani huenda hakukujibu kutokana na ulichokizungumzia.
Pia unatakiwa kuonekana mpya, mwenye mawazo mapya na chanya kila siku. Mbali na kutaka akijibu, lengo jingine ni kumfanya atake au avutiwe kuonana na wewe.
Pia usisahau maswali ya kiuchukozi ambayo yataweza kumfanya atabasamu, mfano, unadhani wewe ungekuwa lugha, ungependelea kuwa lugha gani? Ni swali la kawaida, lakini litamfurahisha na kumfikirisha kabla hajakubu.
Zungumzia mambo chanya
Tumejikita zaidi kwenye kujadil nini usifanye, au nini usiseme. Lakini je? Vipi kuhusu nini cha kusema/kufanya?
Ibua mambo yenye majibu chanya, tumia emojis, memes kwenye simu yako kumshawishi akujibu. Pia usisahau jumbe zenye kumfurahisha. Unatakiwa kujua namna ya kumfanya msichana afurahi kwa kusoma tu ujumbe wako, hadi aanze kutafakari hutu mtu nikiwa nae ana kwa ana itakuwaje kama kwenye simu tu ananifanya nijisikie vizuri hivi.
Lengo ni kutengeneza mazingira ya urafiki wa juu juu kwanza ili akujibu au/na akubali muonane hata kama ataamua kukataa utakachomwambia.
Wasiliana na wasichana wengine
Ili kuweza kumuonesha kuwa hujali sana asipokujibu, lakini pia kukuwezesha na wewe kumsahau kwa baadhi ya nyakati, wasiliana na wasichana wengine ambao watakusaidi usiwe unamuwaza yule unayetaka akujibu.
Huweza ukaumizwa na msichana mmoja kutokukujibu wakati tayari unao wengine watano wanaokujibu na maisha yako yanakwenda.
Wale ambao huenda baa au kwenye kumbi za burudani wanaifahamu hii kanuni. Ili kumpata msichana unayemtaka, huwa wanazungumza na wasichana wengine wengi kwa makusudi ili mlengwa aone wivu, ahisi kwamba akichelewa itakula upande wa dereva.
Endapo baada ya jitihada zote hizi hatokujibu, tambua kwamba kikubwa ni uhai, na kuna jema hata katika mambo mabaya

Jumanne, 10 Desemba 2019

MLONGE SABUNI

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MLONGE


SABUNI YA MLONGE:

MAHITAJI

1:JUISI YA MAJANI MABICHI YA MLONGE ROBO LITA IWE NZITO.( ROJO)


2: CAUSTIC SODA  NUSU KILO

3: MAFUTA ( MISE, MBOSA, ALIZETI, MAWESE NK) LITA MOJA

4: PAFYUMU LEMON
5: MOULD) UMBO
-------------------
JINSI YA KUTENGENEZA:


HATUA YA 01:
LOWEKA CAUSTIC SODA ½ KILO KTK MAJI LITA 2½ KISHA KOROGA KUELEKEA UPANDE MMOJA KWA MUDA WA NUSU SAA KISHA FUNIKA ACHA KWA MASAA 24.( SOLUTION)


HATUA YA 02:
CHUKUA ROJO LA MAJANI YA MLONGE ROBO CHUJA VYEMA IWE SOFTI SANA KISHA MIMINA KTK MAFUTA LITA MOJA,KOROGA KWA DAKIKA 10 KISHA


HATUA 03:  CHUKUA SOLUTION( CAUSTIC SODA NUSU LITA  ULIYOILAZA KWA MASAA24 , MIMINA KTK MAFUTA  CHANGANYA NA ROJO KISHA KOROGA KUELEKEA UPANDE MMOJA HADI IWE NZITO KAMA UJI , WEKA PAFYUM NUSU KIJIKO  CHA CHAI ,KOROGA DAKIKA 5, KISHA MIMINA KTK UMBO( MOLD)

D ULIYOIANDAA.

BAADA YA MASAA 24 ITOE KTK MOULD IWEKE SAKAFUNI ILI IZIDI KUKAUKA VYEMA.

UTENGENEZAJI WA ICE CREAM ZA UBUYU

UTENGENEZAJI WA ICE CREAM ZA UBUYU

10/12/2019
🍦🍦1.ICE CREAM ZA UBUYU🍦🍦

🍦mahitaji:-
  ubuyu wa unga 1/2
  sukari 3/4
  ngano vijiko vi 2. 
  Rangi yoyote
  maji litre8-10
  vannila/hiliki.

🍦🍦Weka maji, weka ubuyu wa unga nusu kilo.  ubuyu changanya kbs na unga wa ngano vijiko viwili.

🍦🍦bandika jikoni huku ukikoroga mpaka uwe mzito kiasi. weka sukari pia chota hata sehemu tatu ili kuweka rangi tofauti. koroga dk 5
then epua pooza na ufunge kwenye vifuko.

N:B Unga wa ngano unafanya ice cream iwe laini isiwe ngumu.
badala ya ngano unaweza weka corn flour. japo ni gharama kdg

Hivyo ndivyo unaweza kutengeneza ice cream ya ubuyu hatua kwa hatua

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA UNGA

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA UNGA

10/12/2019
JE UNGEPENDA KUJUA
JINSI YA KUTENGENEZA
SABUNI YA UNGA???

   Karibu uungane nami
katika mafunzo haya
leo tutajifunza utengene
zaji wa sabuni ya unga
     Mahitaji
1)Saifonic acid kilo 1
2)Maji nusu lita
3)Soda ash kilo 6
4)Sodium metassilyket
    kilo 1
5)Optic blaitina vijiko 10
    vya chakula
6)Perfume vijiko 2 vya
    Chakula
7)Rangi vijiko 2 vya
    chakula
8)Nanza
 
       Hatua
1)Andaa ndoo ya plastik
kisha tia sallifonic acid
na uanze kukoroga
kuelekea upande mmoja

2)Tia optic blaitina ,nanza
  na perfume na uendelee
kukoroga mpaka vichanganyikane
Vizuri

3)Wakati unaendelea kukoroga
tia soda ash nusu na uendelee kukoroga kisha
tia sodium metasilic yote na ukoroge
mpaka vichanganyikane vizuri

4)Tia rangi vijiko 2 vya chakula,halafu tia maji na koroga vichanganyikane vizuri
baada ya hapo anika sabuni yako kivulini  kwa
kutumia nailon kwa muda wa masaa matatu au manne baada ya hapo sabuni
itakuwa tayari kwa matumizi

Huo ndio utengenezaji wa sabuni ya unga hatua kwa hatua

Asante sana na usiache kunifuatilia katika muendelezo wa mafunzo haya ya utengenezaji wa bidhaa za viwandani

Endelea kutembelea blog hii utafaidika sana
 Kwa mawasiliano zaidi piga
 0675037995

Jumatatu, 15 Aprili 2019