Jumatatu, 24 Septemba 2018

Raisi magufuli ndani dreamliner


Usivunje uhusiano kwa sababu Umepata abayekufaa

*Usivunje uhusiano na mtu sababu tu umegundua kuwa sio rafiki.* Kwenye maisha hatuhitaji marafiki tu. Tunahitaji watu wote.

Kila mtu atakufaa kwa namna tofauti. Hata wale wasio marafiki, kuna kipindi watakufaa.

Sio kila mtu atakufaa kwenye biashara au kipindi unatafuta kazi.
Na sio kila mtu atakufaa kipindi unajiandaa na harusi yako au kipindi unatafuta mtu wa kukukopesha.

Pia, sio kila mtu atakufaa kipindi unaumwa au kipindi umefiwa.

Jambo moja tunalokosea ni kudhani kuwa *yupo mtu atakayetufaa kwa kila kitu.* Na kwa namna hiyo, tumepoteza watu wengi ambao wangekua na manufaa kwetu. *Anaekufaa kwa kila kitu ni Mungu pekee.* Binadamu wote watakufaa tu kwa msimu.

Kinachotakiwa ni kutambua kila mtu anaekuzunguka anakufaa kwa nini, na kumtumia kwa hicho ambacho anakufaa. *Usivunje urafiki wa miaka mitano sababu tu hakuja kwenye msiba ulipofiwa.* Ndani ya miaka mitano, hakukufaa kwa jambo jingine lolote lile?

Chumvi haitakufaa kwa chai asubuhi, ila itakufaa kwa mboga mchana.

Kila mtu atakufaa katika jambo tofauti na katika nyakati tofauti.

Mahusiano bora huongozwa na akili na si hisia

Jumapili, 23 Septemba 2018

Hapo zamani mambo yalikuwa hivi


Hamissa Mobetto Ataja Sababu za Kublock Diamond

Hamissa Mobetto Ataja Sababu za Kublock Diamond

Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameeleza sababu ya kum-block Diamond Platnumz kwenye ukurasa wa Instagram wa mwanae.

Kwenye Mahojiano na The Playlist ya Times FM, Hamissa amesema amefikia uamuzi huo kutokana na Diamond kumuingiza mtoto kwenye mambo yao na pia kushindwa kumuheshimu.

"Kwenye page ya mtoto sio kumfuta tu mpaka kum-block kwa sababu anakuwa kama mtu hajielewi, hata we have issues usimuingize mtoto ama mama mtoto wako,' amesema.

"Unajua sisi kwetu wanasema jitahidi umsitiri mtu aliyekuzalisha, mtu uliyemzalia ama mke wako wa ndoa, mume wako wa ndoa kwa sababu aibu yake ni ni yako pia," amesema Hamisa Mobetto.
 
Hamisa Motto ni mama wa watoto wawili, mmoja akiwa amezaa na Diamond Platnumz.